Wakazi wa Mtaa wa
Tambuka reli Kata ya Mpanda Hotel Manispaa ya Mpanda wamelalamikia
uongozi wa kata hiyo kwakutopewa lisiti pindi wanapotozwa faini za usafi.
Wakizugumza na mpanda
radio wakazi hao wamesema wamekuwa wakilipa faini kwaajili ya uchafu ambao upo
katika maeneo yao lakini hawapewi lisiti.
Aidha wamesema kuhusu
gari la taka limekuwa likifika katika eneo hilo lakini taka bado haziondolewi,
na kuiomba serikali kuingilia kati suala hilo kwani taka hizo zinaweza
kusababiasha magonjwa ya mlipuko.
Mpanda radio imemtafuta
AfisaMtendaji wakata hiyo ili aweze kuzungumzia madai ya wananchi kulipishwa
faini na kutopewa lisiti lakini hakupatikana.
Maeneo mengi katika
manspaa ya Mpanda bado kuna changamoto kubwa ya usafi hususani katika suala la
uondoaji wa taka katika maeneo ya makazi ya watu.
Chanzo:Johari Secky
No comments:
Post a Comment