Wananchi wilayani Mpanda Mkoani Katavi wametakiwa kuwa wavumilivu wakati wa zoezi la kujiandikisha kwa ajili ya kupata vitambulisho vya taifa likiendelea
Kauli hiyo imetolewa na Zamalad Athman Mbangwa
ambaye ni afisa msajili Msaidizi wilaya ya Mpanda wakati akizungumza na Mpanda
Radio kuhusu zoezi la wananchi kujiandikisha kwa ajili ya vitambulisho hivyo.
Aidha amesema wananchi ambao walishajiandikisha
katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo watapewa taarifa vitambulisho
vitakapokuwa vimekamilika.
Hivi karibuni wakazi wa kata ya Kapalala
Halmshauri ya wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi,waliiomba mamlaka ya vitambulisho nchini NIDA
kubainisha lini vitambilisho hivyo vitapatikana.
Zoezi la uandikishwaji wa vitambulisho vya Taifa
bado linaendelea mkoani Katavi ambapo kwa mjibu wa NIDA vinatarajiwa kukamilika
mwezi Septemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment