Baadhi ya wakazi katika Kijiji cha Matandalani Kata ya Stalike Mkoani Katavi wamesema wanapata fursa ya kuwahoji viongozi wao juu ya
maendeleo licha ya hoja zao kutofanyiwa kazi kwa wakati.
Wakizungumza na Mpanda Redio wakazi hao wamesema ni kwa muda
mrefu hawajishughulishi na kilimo kutokana na kuwaondolewa katika eneo la
hifadhi na kutofahamu hatima ya suala hilo mpaka sasa.
Adha hiyo imekwamisha
maendeleo katika kijiji hicho kwani wengi wao wamekuwa wakitegemea kilimo kwajili ya kujikwamua kiuchumi .
Wakazi wa Kijiji cha Matandalani kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakijishughulisha na kilimo lakini
kwasasa baadhi yao wamehamia kwenye shughuli za machimbo ambazo zinaonyesha
kutokidhi mahitaji yao.
Chanzo:Ester Baraka
No comments:
Post a Comment