Wito umetolewa kwa
Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini
kuwahimiza waumini kufanya usafi
katika maeneo ya makaburi.
Hayo yamebainishwa na
mstahiki meya wa manispa ya Mpanda Willium Mbogo ambapo amewataka wauminini
wote kukumbuka kufanya usafi na kuweka mazingira mazuri katika maeneo ambayo
wanatumia kuzika .
Aidha amesema makaburi
mengi kwa sasa yamezungukwa na majani ambazo zimeleta vichaka hali ambayo
inashusha vigezo vya usafi kitaifa hivyo kila mtu aone umuhimu wa kujali maeneo
hayo.
Tatizo la usafi katika
maeneo mbalimbali mkoani Katavi bado ni changamoto kutokana na mwamko mdogo wa
wananchi katika usafi wa mazingira.
Source:Rebacca
kija
No comments:
Post a Comment