Wakati serikali ikihimiza
matumizi ya vyandarua ili kujikinga na ugonjwa wa Maralia baadhi ya Vijana wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi wanavua samaki kwa kutumia
vyandarua Katika mto Mpanda.
Katika Mahojiano vijana hao
ambao hawakuwa tayari kujitambulisha wamedai kutumia vyandarua hivyo ili
kurahisisha upatikanaji wa kitoweo cha Samaki.
Mto huo ambao unadaiwa kuwa
chanzo cha jina Mpanda umezongwa na shughuli lukuki za kibinadamu ambazo
huhatarisha, mazingira hata kuwepo kwa kitisho cha magonjwa ya mlipuko.
Diwani wa Kata ya Misunkumilo Matondo
Alfred amesema anafanya kila liwezekanalo ili kuchukua hatua dhidi ya vijana
hao.Katika
nchi za Afrika Mashariki inakadiriwa kuwa na wagonjwa milioni 60 na watu
milioni moja huripotiwa kufa duniani kila mwaka.
Source:Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment