Baadhi ya Wajasiriamali
halimashauri ya manispaa ya mpanda wamelilalamikia shirika la pride Tanzania
mkoani Katavi linalojihusisha na utoaji wa mikopo kushindwa kuwalipa gawio la
fedha kwa muda wa miezi minne sasa.
Wakizungumza na Mpanda Redio
kwa nyakati tofauti wamesema madai yao ni zaidi ya shilingi milioni moja tangu
mwezi wa kumi mwaka jana lakini mpaka sasa hawajalipwa fedha hizo licha ya
kufuata masharti ya marejesho ya mikopo kwa wakati kwenye shirika hilo.
Aidha wamesema malalamiko yao
yamefikishwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kupata ufumbuzi jambo ambalo mpaka
sasa halijatatuliwa.
Kwa upande wa Meneja wa Pride Mkoa wa Katavi Ambele Chamba amesema anafuatilia ili kujua ukweli wa madai hayo
yafanyiwe kazi.
Chanzo:Paul mathias
No comments:
Post a Comment