Haki miliki ya pichaImage captionUturuki na Marekani katika mzozo wa utoaji visa
Uturuki na Marekani wamekuwa kwenye mzozo wa kibalozi ambapo huduma kadha za visa zimesitishwa.
Ubalozi wa Uturuki mjini Washington ulisema kuwa ulitaka kutathmini kujitolea kwa serikali ya Marekani kwa usalama wa ubalozi wake na wafanyakazi wake.
Taarifa kama hiyo ilikuwa imetolewa mapema na ubalozi wa Marekani mjini Ankara.
Hii inajiri baada ya mfanyakazi wa ubalozi wa Marekani mjini Instabul kushikwa wiki iliyopita, kwa kushukiwa kuwa na uhusiano na kiongozi wa dini anayedaiwa kuhusika kwenye jaribio la mapinduzi lililofeli mwaka uliopita nchini Uturuki.
Marekani ililaani hatua hiyo kuwa isiyo na msingi na inayohujumu uhusiano kati ya nchi hizo.
Haki miliki ya pichaImage captionFethullah Gulen
Mfanyakazi aliyekamatwa alikuwa ni mwanamume raia wa Uturuki.
Ubalozi wa Marekani ulisema kuwa huduma za visa zisizo za kuhamia Marekani nchini Uturuki zimesitishwa.
Visa zisizokuwa za kuhamia kabisa Marekani ni kama zile za kitalii, za kutafuta matibabu, za kibiashara na ajira ya muda na masomo.
Wale wanaotaka uraia au kuishi Marekani huomba visa za kuhamia Marekani.
Uturuki kwa miezi mingi imekuwa ikiishinikiza Marekana kumsalimisha kiongozi wa dini Fethullah Gulen, kwa madai ya kuhusika kwenye jaribio la mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2016.
Baadhi
ya Wakazi mjini mpanda Mkoani Katavi wakiwemo wafanyabiasha wameliomba shirika la umeme Tanzania
(TANESCO) Mkoani Katavi Kuboresha miundombinu yao ili kukomesha tatizo la
kukatika umeme mara kwa mara mjini hapa.
Wakiongea
na mpanda radio leo baadhi ya wakazi hao
wamesema umeme ndio nyenzo kubwa ya kuendesha shughuli zao hivyo kukatika kwake
kunaathiri hali ya kipato kwa kila mmoja.
Katika
taarifa yake aliyoitoa hivi karibuni Afisa
uhusiano wa Shirika hilo mkoani Katavi bwana Amoni Michel Bidebuye amekiri kuwepo changamoto hiyo na kuahidi
kuendelea kuzitatua kwa nguvu zote.
Licha
ya TANESCO mkoani katavi kuboresha mitambo yao ya kuzalisha umeme, shirika hilo
bado halijaweza kufanikiwa kutoa umeme wa uhakika kwa wateja wake.
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi. Lilian
Matinga amesema atawasiliana na idara zinazohusika na wanyama Mkoani Katavi ili
kushughulikia tatizo la viboko wanaotishia maisha ya wakazi wa kijiiji cha
Milala na kuharibu mazao shambani.
Matinga ametoa kauli hiyo leo wakati
akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusu
viboko hao waliopo bwawa la milala.
Wiki iliyopita,wakazi wengine
waliolalamikia uharibifu unaofanywa na viboko hao,wanaishi mitaa ya Kigamboni
na Makanyagio ambapo,waliilalamikia serikali kutochukua hatua za kuwadhibiti viboko
ambao wamesababisha pia baadhi ya ndoa kuvunjika kutokana na wanaume kuhamishia
makazi yao shambani ili kukabiliana na wanayama hao.
Bwawa la milala ambalo ni miongoni
mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda, linasemekana
kwa sasa lina viboko zaidi ya thelathini.
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe kuwapeleka maofisa wa Makumbusho mpya ya Olduvai Gorge jijini Dubai kwa ajili ya mafunzo zaidi ya kiteknolojia. Samia alitoa maagizo hayo wakati akizindua rasmi majengo ya Makumbusho mpya ya Olduvai Gorge ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, mradi uliojengwa kwa gharama ya Sh bilioni 1.7 huku asilimia 80 ya gharama hizo zikiwa ni ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU) na kiasi kilichobaki ni fedha kutoka Serikali ya Tanzania.
“Tuna Makumbusho kubwa zaidi barani Afrika yenye kuweza kutoa historia ya Zamadamu, yaani binadamu wa kale, maisha na zana zake; lakini hii itakuwa bora zaidi ikiwa tutaifanya iwe kiteknolojia zaidi,” alisema Makamu wa Rais, na kuongeza kuwa Waziri Maghembe kupitia uhusiano mzuri alionao na nchi za Saudi Arabia, atafanikisha suala la kuwapeleka wataalamu kwenda kupata mafunzo zaidi Dubai.
Makamu wa Rais pia ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kujenga makumbusho kwenye maeneo mengine ya kihistoria kama Kilwa (Lindi), Amboni (Tanga), Bagamoyo (Pwani) na Zanzibar maana kwa sasa mwelekeo wa watu wengi duniani ni kurudi nyuma wajionee jinsi dunia ilivyokuwa zamani.
Kwa upande wake, Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Maghembe alisema Makumbusho ya Olduvai Gorge ni ya pekee duniani ambapo karibu kila zana za kale, mabaki ya zamadamu na alama halisi zilizoachwa na binadamu zaidi ya miaka milioni 4 iliyopita, vinapatikana; “Hakuna kama hii ulimwenguni kote.”
Naye Mbunge wa Ngorongoro ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, William Ole Nasha ameuomba uongozi wa Wilaya ya Ngorongoro pamoja na Mamlaka ya Hifadhi kuangalia matumizi bora ya ardhi katika eneo hilo ambalo lina mchanganyiko wa hifadhi ya wanyamapori, wafugaji wa jamii ya Kimasai na eneo la historia ya mambo ya kale.
“Na katika kila faida inayoongezeka kupitia Utalii, tungependa kuwa wakazi wa eneo hili pia wawe wananufaika zaidi,” alisema Ole Nasha. Meneja wa Urithi wa Utamaduni katika Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, Joshua Mwankunda alisema Makumbusho ya Oldupai ni moja kati ya mipango mingine mikubwa inayotarajiwa katika eneo hilo, ukiwemo ule wa Makumbusho katika eneo jirani la Laetoli ambako nyayo za binadamu wa kale aliyeishi eneo hilo miaka milioni 4 iliyopita zinapatikana.
Waziri wa Elimu, Sayansi ya Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako
SERIKALI imeeleza kwamba matatizo ya Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ni kulipwa kwa wanafunzi hewa, ubadhirifu wa fedha na kuwepo kwa watendaji wanaohusika kuweka fedha za wanafunzi wanne kwa mwanafunzi mmoja.
Kadhalika imeeleza tabia ya HESLB kujiona ‘Mungumtu’, kuwaona watoto wa Watanzania kama ni shida kwaona wasiostahili kupewa mikopo na hata kuwa na majibu ya mkato yasiyokuwa na chembe ya kazi ya utoaji huduma. Waziri wa Elimu, Sayansi ya Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua Bodi mpya ya HESLB na kuitaka kujitenga na menejimenti wakati wa utekelezaji wa majukumu yake na kuhakikisha matatizo hayo yote ambayo yapo katika taarifa aliyowakabidhi, yanakaguliwa upya, kuhakikiwa na kufanyiwa kazi.
Pia alisema taarifa hiyo imeambatanisha taarifa ya fedha za HESLB zilizochezewa. Alikabidhi taarifa hiyo kwa Makamu Mwenyekiti wa bodi mpya, Madina Mwinyi akiagiza ifanyiwe kazi kuhakikisha na kujiridhisha pamoja na kuwajua wadeni wa HESLB huku ikiepuka kuiamini menejimenti kama ilivyokuwa kwa bodi ya awali badala yake kuisimamia. “Ninakabidhi taarifa yenye changamoto za Bodi ya Mikopo kwenu Bodi ya Wakurugenzi ambayo inaainisha uwepo wa wanafunzi hewa na ambao wanalipwa mikopo wakiwemo waliomaliza au kuacha chuo,” alisema.
Pia alisema taarifa hiyo inahusisha kuwepo kwa watendaji wanaohitajika kujieleza ambao walikuwa wakiweka fedha za wanafunzi wanne kwa mwanafunzi mmoja ambapo ushahidi upo na eneo hilo bado kuna shida. Kadhalika, aliiagiza Bodi mpya kutazama upya na kujiridhisha kuhusu vigezo vya utoaji mikopo kwani kumekuwa na matatizo, na hata kutizama utoaji wa mikopo kama taratibu na sheria zinazingatiwa. “Malalamiko ya Bodi ya Mikopo yapunguzwe ama kuondolewa kabisa ili kukidhi matarajio ya wadau wa elimu nchini, endeleeni kukagua na hata majina ya wanaohitajika kupata mikopo kabla ya kutolewa rasmi,” alisema Profesa Ndalichako.
Kuhusu Bodi mpya aliitaka isimamie zaidi urejeshwaji wa mikopo kwani hadi sasa serikali imetoa Sh trilioni 3.1 tangu kuanzishwa kwa bodi, lakini ni Sh milioni 217 pekee zilizorejeshwa huku Sh bilioni 588 zikiwa zimefikia muda wake zikitakiwa kulipwa. Akizungumza baada ya bodi hiyo kuzinduliwa, Makamu Mwenyekiti, Madina Mwinyi alisema katika kufanyia kazi changamoto za HESLB wataanza kwa kujipanga wao wenyewe katika taasisi wanamotoka ili kila mmoja kujua ni kiwango gani cha mikopo kinachotakiwa kurejeshwa.
Kadhalika alisema bodi hiyo itahuisha taswira ya HESLB pamoja na kuiaminisha jamii kuwa suala la mkopo wa elimu ya juu ni lazima kurejeshwa kwa wakati. Wajumbe wa bodi hiyo na taasisi wanazotoka katika mabano ni Profesa Caroline Nondo (Mwakilishi kutoka Tume ya Vyuo Vikuu), Susan Urio (Mwakilishi wa Wanafunzi), Madina Mwinyi ambaye ni Makamu Mwenyekiti (Mwakilishi wa Wizara ya Elimu Zanzibar).
Wengine ni pamoja na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Gerson Mdemu (Mwakilishi wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali), Dk Dalmas Nyaoro (Mwakilishi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia), Frank Mgeta (Mwakilishi wa Wizara ya Fedha na Mipango), Dk Francis Masika (Mwakilishi wa Baraza la Elimu ya Ufundi) na Mjumbe mmoja ambaye ni Mwakilishi wa Wizara ya Fedha Zanzibar hajateuliwa.
Pia, amesema kwamba madiwani ambao hawaridhiki na kiwango cha posho cha Sh 350,000, wajiuzulu kwa kuwa kwa sasa serikali haiwezi kuongeza kiasi hicho cha fedha. Akifungua Mkutano Mkuu wa 33 wa ALAT Dar es Salaam jana, Rais Magufuli alisema anatambua kazi kubwa inayofanywa na mamlaka za Serikali za Mitaa kwa sababu hata kwenye ukaguzi wa vyeti vya watumishi wa umma, wao ndio waliosaidia kazi hiyo kwenda vizuri na kufanikiwa kwa kuwaondoa watumishi hewa zaidi ya 20,000.
Kwa mujibu wa Rais Magufuli, watumishi hewa walikuwa wanaigharimu serikali Sh bilioni 19.848 kwa mwezi na kwa mwaka Sh bilioni 238.176, wakati wafanyakazi waliokuwa na vyeti feki walikuwa 12,000 na waliigharimu serikali Sh bilioni 11.9 kwa mwezi na kwa mwaka Sh bilioni 142.9, hivyo kwa mwaka gharama iliyokuwa inatumika kuwalipa wenye vyeti feki na wafanyakazi hewa ilikuwa Sh bilioni 381. Mbali na wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, Rais alisema pia zilikuwepo kaya hewa na wanafunzi hewa ambavyo vyote vilikuwa mianya ya kufuja fedha za umma.
Dk Magufuli aliongeza kuwa kulikuwa na kaya hewa 57,000 na wanafunzi hewa 65,000. Rais alisema mifumo hiyo ya kufuja fedha za umma, kwa sasa imedhibitiwa na kuongeza nidhamu na weledi kwenye utumishi wa umma. Kuhusu posho hizo za madiwani, Rais Magufuli aliwakumbusha wajumbe kuwa wakati walipogombea udiwani, walijaza fomu maalumu ambayo moja ya vipengele vilimtaka diwani awe na kazi maalumu ya kumwingizia kipato. Alisema kama wapo madiwani waliojaza fomu hii na hawana kazi ya kuwapatia kipato, wajiuzulu udiwani.
“Ninyi ndio wasimamizi wa miradi, mafanikio tuliyoyapata kwa miezi hii 23, pia yanatokana na mchango wenu. Mlisimamia vizuri suala la madawati, lakini bado kuna changamoto ya upungufu wa madarasa, nyumba za walimu, vyoo, nawaomba mkatatue matatizo haya, himizeni wananchi kuwapeleka watoto shule,” alieleza Rais Magufuli. Rais Magufuli aliwataka wajumbe wa mkutano huo pamoja na wakuu wengine wa mikoa, kujifunza ubunifu alionao Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda namna anavyofanya kazi zake.
Alisema Makonda amekusanya Sh milioni 180 kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwenye mkoa wake. Katika mkutano huo, Makonda aliwaomba wajumbe wamchangie mifuko ya saruji. Alisema wananchi wanaposhirikishwa kuchangia mambo ya maendeleo hawana shida, tatizo linakuja kwenye namna fedha hizo zinavyotumika. Aliwataka wakurugenzi, madiwani, mameya na wenyeviti wa halmashauri, kusimamia vyema fedha za wananchi katika kuwaletea maendeleo.
Mkosoaji mkubwa wa rais wa Rwanda Paul Kagame, Diane Rwigara ameshtakiwa kwa kuchochea uasi dhidi ya serikali.
Ameshtakiwa pamoja na mama yake Adeline Rwigara na dada yake Anne Rwigara.
Diane Rwigara aluzuiwa kuwania urais wa mwezi Agosti nchini Rwanda.
Rais wa sasa Paul Kahame alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 99, na kupelekea madai kuwa kuikuwa na udanganyifu madai yalipingwa na mamlaka ya nchi hiyo.
Diane Rwigara pia ameshtakiwa kwa kubuni stakabadhi bandia.
Wachunguzi wanadai kuwa Bi Rwigara alivunja sheria za uchaguzi kwa kukusanya sahihi bandia kuunga mkono ugombeaji wake.
Haijulikani ni kitu gani kilichangia afunguliwe mashtaka ya kuchochea uasi.