MPANDA
Mkuu wa wilaya ya Mpanda Bi. Lilian
Matinga amesema atawasiliana na idara zinazohusika na wanyama Mkoani Katavi ili
kushughulikia tatizo la viboko wanaotishia maisha ya wakazi wa kijiiji cha
Milala na kuharibu mazao shambani.
Matinga ametoa kauli hiyo leo wakati
akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake kuhusu malalamiko ya wananchi kuhusu
viboko hao waliopo bwawa la milala.
Wiki iliyopita,wakazi wengine
waliolalamikia uharibifu unaofanywa na viboko hao,wanaishi mitaa ya Kigamboni
na Makanyagio ambapo,waliilalamikia serikali kutochukua hatua za kuwadhibiti viboko
ambao wamesababisha pia baadhi ya ndoa kuvunjika kutokana na wanaume kuhamishia
makazi yao shambani ili kukabiliana na wanayama hao.
Bwawa la milala ambalo ni miongoni
mwa vyanzo vya maji yanayotumika kwa wakazi wa Manispaa ya Mpanda, linasemekana
kwa sasa lina viboko zaidi ya thelathini.
No comments:
Post a Comment