Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameagiza taasisi za Serikali na taasisi binafsi zinazotumia mifumo ya kielektroniki kujiunga na mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki (Electronic Revenue Collection System {e-RCS}) ili kupata taarifa za uhakika na kulinda usalama wake pamoja na kuiwezesha Serikali kukusanya mapato yote stahiki.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 01 Juni, 2017 alipotembelea Kituo cha Taifa cha Kuhifadhi Kumbukumbu (National Internet Data Center) kilichopo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam na kisha kuzindua mfumo wa ukusanyaji wa kodi kwa njia ya kielektroniki uliotengenezwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) kwa kutumia wataalamu wa ndani.
Uzinduzi huo umehudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mawaziri na Makatibu Wakuu wa Tanzania Bara na Zanzibar na wadau mbalimbali wakiwemo wawakilishi kutoka benki mbalimbali, kampuni za simu na viongozi wa dini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akihutubia baada ya wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na na kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akihutubia katika Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) wakati wa kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) Bw. Joseph Kichere wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akisalimiana na Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa shirika la simu Tanzania TTCL Bw. Waziri Kindamba wakati wa kutembelea Kituo cha Kutunzia Taarifa (Data centre) na kuzindua Mfumo wa Ukusanyaji Mapato wa Serikali kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akionesha Ipad maalumu aliyopewa ili kumuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na kushoto kwake ni Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein akionesha Ipad maalumu aliyopewa kumuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. kushoto kwake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine wakati wa kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan akionesha Ipad maalumu itayomuwezesha kufuatilia ukusanyaji wa mapato ya kila siku. Kulia kwake ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Ali Mohamed Shein na viongozi wengine wakati wa kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akishuhudiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akizindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa makampuni ya mawasiliano mbalimbali nchini kwenye sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa Mabenki mbalimbali nchini sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi katika picha ya pamoja na wakuu wa Mabenki mbalimbali nchini sherehe ya uzinduzi wa Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akitoka kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaa
m leo June 1, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli akiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein na Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan na viongozi wengine akitoka kutembelea kituo cha kutunzia taarifa (Data Centre) kabla ya kuzindua Mfumo wa Serikali wa Ukusanyaji Mapato kwa Njia ya kielektroniki kwenye sherehe zilizofanyika Kijitonyama jijini Dar es salaam leo June 1, 2017.
Picha na Ikulu
No comments:
Post a Comment