Inspekta Jenerali wa Jeshi la
Polisi, IGP Simon Sirro amesema kuwa jeshi hilo halitachukua muda kuwatia
nguvuni kikundi cha uhalifu wa mauaji ya
baadhi ya askari, raia na viongozi wa wilaya za Kibiti, Mkuranga na Rufiji
katika Mkoa wa Pwani.
IGP Sirro akiongea na waandishi wa habari |
IGP Sirro ametoa onyo hilo leo
Mei 31, 2017, wakati akizungumzia mikatati yake ya kutokomeza mauaji hayo,
ambapo ametangaza dau la shilingi milioni 10 kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa
sahihi zitakazosaidia jeshi hilo kukamata wahalifu hao.
Ameeleza kuwa, Jeshi hilo linapanga kukutana na wananchi wa
maeneo hayo hivi karibuni ili kuzungumza nao juu ya matukio yaliyotokea kwa
lengo la kupata ushirikiano wao, na kuwatoa hofu.
Ameongeza kuwa nguvu inayotumiwa na jeshi hilo sasa ni za
mpito katika kuhakikisha linarudisha amani, na kuwataka raia wema kutokimbia
makazi yao.
Pia
IGP Sirro amewatangazia kiama madereva wa bodaboda na kuwataka kuacha kuvunja
sheria za barabarani kwa makusudi huku akisisitiza utii wa sheria bila shuruti.
No comments:
Post a Comment