Sunday, 25 June 2017

WAISLAMU WATAKIWA KUTENDA MEMA HATA BAADA YA MFUNGO WA RAMADHANI KUISHA

                                    Katibu wa Bakwata wilaya ya Mpanda Omari Munna




       MPANDA

Kesho ni siku kuu ya Eid el fitr

Waislamu mkoani katavi wametakiwa kuendelea kutenda yaliyomema na kuyaacha yasiyofaa hata baada ya kumaliza mwezi mtukufu wa ramadhani

Rai hiyo imetolewa na katibu mkuu wa bakwata wilaya ya mpanda Omari Muna wakati akizungumza na mpanda redio ofisi kwake juu ya maandalizi ya swala ya eid 

Muna amesema kwa imani dini hiyo endapo yeyote atafanya maaswi siku ya eid ni sawa na kumkosea mtume siku ya kiama

Swala ya Eidi  inatarajiwa kuswaliwa kesho saa moja asubuhi  na baraza la Eid  saa 9 alaasiri,  kimkoa linatarajiwa kufanyika katika viwanja vya shule ya msingi Kashaulili na mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa wa Katavi meja Jenerali Mstaafu Rafaeli Muhuga



No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...