Bradley alitembea kwenye zulia jekundu wakati wa hafla ya Tuzo za Mchezaji Mashuhuri wa Mwaka wa BBC 2016 |
Shabiki wa klabu ya Sunderland wa umri wa miaka sita Bradley Lowery, ambaye tatizo lake la kiafya liligusa nyoyo za wengi amefariki dunia. Bardlaye alikuwa anaugua ugonjwa ambao wa Kiingereza hufahamika kama neuroblastoma - aina nadra ya saratani - tangu alipokuwa na umri wa miezi 18.
Bradley alifanywa kuwa kibonzo-nembo wa klabu hiyo na akaunda urafiki wa karibu na mshambuliaji wa klabu hiyo Jermain Defoe
Aidha, aliongoza wachezaji wa England kuingia uwanjani Wembley
wakati wa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Lithuania.
Kifo chake kimethibitishwa na wazazi wake kwenye mitandao ya
kijamii. "Kijana wetu mkakamavu ameenda kuwa na malaika leo. "
Alikuwa shujaa wetu na alipigana sana lakini alihitajika kwingine.
Hatuna maneno ya kueleza jinsi tulivyohuzunishwa na kifo chake."
Bradley alipewa matibabu lakini saratani yake ikaibuka tena mwaka
jana. Wahisani walichangisha zaidi ya £700,000 kulipia matibabu yake New York
mwaka 2016, lakini madaktari waligundua kwamba saratani yake ilikuwa imeenea
sana na hangeweza kutibiwa.
Bradley na babake Carl mechi kati ya Everton na Sunderland |
Bradley aliipenda sana Sunderland na aliruhusiwa kuingia uwanjani Stadium of Light |
Wazazi wake Gemma na Carl, kutoka Blackhall Colliery, Durham,
waliambia Desemba kwamba alikuwa amesalia na "miezi kadha tu ya
kuishi".
Miezi minne baadaye, walifahamishwa kwamba jaribio la mwisho
kabisa la kumtibu lilikuwa limefeli.
Bradley alikuwa kibonzo-nembo wachezaji wa England wakiingia uwanjani kucheza
dhidi ya Lithuania mwezi Machi Bradley Lowery.
Bradley alipendwa na maelfu ya watu na alipokea kadi 250,000 za
kumtakia heri wakati wa Krismasi, kutoka kwa watu mataifa ya mbali kama vile
Australia na New Zealand.
Defoe aliunda urafiki na Jermain Defoe enzi za uhai wake habari kutoka Bbc swahili.
No comments:
Post a Comment