Friday, 7 July 2017

TABIA YA BAADHI YA WAZOA TAKA KUTUPA UCHAFU MAKABURINI BADALA YA KUUPELEKA KWENYE VIZIMBA.

Wakazi wa mitaa ya Fimbo ya Mnyonge na Mwangaza, kata ya Makanyagio katika Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi wameonyesha kuchukizwa na tabia ya baadhi ya wazoa taka kutupa uchafu huo makaburini badala ya kuupeleka kwenye vizimba.

Wamesema kuwa utaratibu wa kuwepo na vikundi vya ukusaji taka ni mzuri na umewapunguzia kero isipokuwa unaharibiwa na watu wachache wanaotupa taka hizo katika makaburi ya Mwangaza.

Akiongea na Mpanda Radio leo kwa niaba ya wananchi wa maeneo hayo khamis khamis amepongeza juhudi za serikali na kutaka watu wasiowaaminifu kuchukuliwa hatua.

Mwananchi khamis khamis akisema "hilo lipo hata mimi mwenyewe nilipita makaburini kama siku mbili nilipita nikakuta toroli walikuwa wanamwaga taka pale makaburini nam mpaka sasa taka zipo lakini mtaani taka hazipo hao wanakikundi sio waaminifu na sio watu wazuri kwan badala ya kwanda kuwaga sehemu husika wanamwaga makaburini hivyo wanaweza sababisha mfumuko wa magonjwa ya mlipuko". Bwana khamis khamis akizungumza swala utupaji taka makaburini.

 Akiongelea tabia ya utupaji taka Makaburini Mwenyekiti wa mtaa wa Mwangaza Kharili Robert amewaonya wanavikundi kuacha tabia hiyo, kabla hatua za kisheria hazijachukuliwa kwa atakayebainika. Mwenyekiti wa mtaa wa Fimbo ya Mnyonge Bwana kharili Robert alisema "wapo wengine ambao wanapita mitaanina matoroli yao wanachukua takataka wanaenda kutupa makaburi endapo tunawakamata tunawapeleka kwenye kata wanalipishwa faini ya shilingi elfu hamsini pia ambao bado wanaoendelea na tabia kutupa taka.

 Akiendelea kusema Mimi mwenyekiti wa serikali ya kata ya mwangaza nipo tayari kuwachukulia hatua wanaotupa taka makburini pia nawaomba wanachukua taka kuzifikisha kwenye vizimba vilivyoweka." Bwana Khalili Robert alisema.

Aidha amewataka wananchi kutoa taarifa za kufanikisha kuwafichua wenye tabia hizo za utupaji wa taka maeneo ya makaburini ili kuweka mazingira ya mtaa kuwa safi.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...