Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako ameeleza kushangazwa na hatua ya TAMISEMI kupangia wanafunzi 144 wa kidato cha tano mwaka huu, Shule ya Mwandiga mkoani Kigoma ambayo bado haijakidhi vigezo na kupata usajili. Aliyasema hayo tarehe 7 mwezi was saba mwaka 2017
Kufuatia swala hilo waziri ameagiza wakaguzi kufanya ukaguzi kwa nchi mzima katika shule mpya zilizopangiwa wanafunzi wa kidato cha tano kuona kama zinakidhi vigezo au la.
Amesema udhibiti wa ubora wa viwango unapaswa kufanywa pia serikalini na si kwa shule binafsi pekee na kwamba ndiyo maana shule nyingi za serikali zimekuwa hazifanyi vizuri kutokana na kufumbiwa macho.
Aidha amesema serikali imekusudia kuongeza muda wa mwezi mmoja kwa wanafunzi wanaoripoti kidato cha tano lengo likiwa ni kujipanga zaidi hasa kwa shule mpya zilizopandishwa hadhi.
Hata hivyo ameonya wakaguzi kutosita kuchukua hatua pale inapogundua shule imeanzishwa kinyume cha utaratibi huku akitaka kutokuwa na muingiliano wa kimajukumu kati ya wizara yake na TAMISEMI.
No comments:
Post a Comment