Sunday, 9 July 2017

Halmashauri zote zaagizwa kushusha bei za dawa na kuuza kwa bei elekezi.

                  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu 


Halmashauri zote nchini zimeagizwa kushusha bei ya dawa na kuziuza kulingana na bei elekezi inayowekwa kwenye vitabu vya Bohari ya Dawa (MSD). Ailyasema hayo tarehe 7 mwezi wa saba.

Agizo hilo linatokana na kushuka kwa bei za dawa na vifaa tiba kufuatia uamuzi wa serikali kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji badala ya kutumia watu wa kati ‘madalali.'

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ndiye aliyetoa agizo hilo huku akisema hatua ya ununuaji wa dawa kwa wazalishaji moja kwa moja ni utekelezaji wa agizo la Rais Dkt. John Magufuli.

 Waziri Ummy amesema utekelezaji wa ununuaji wa dawa kwa wazalishaji unatekelezwa na MSD ambayo imeingia mkataba na wazalishaji 73 ambapo kumi ni wa nchini na wengine 46 ni wa nje ya nchi ikiwemo Kenya.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu amekiri kuwa kumekuwa na shida ya upatikanaji wa taarifa za mahitaji sahihi na wakati mwingine kupata tafsiri ya kutokuwepo kwa dawa kwenye vituo vya afya.

 Hata hivyo Wizara ya afya imeendelea kusisitiza kuwa dawa hazitolewi bure hivyo wananchi wanatakiwa kuchangia isipokuwa kwa yale makundi maalum pekee.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...