Friday, 7 July 2017

KUSHUKA KWA MAZAO YA NAFAKA YAKIWEMO MAHINDI NA MPUNGA WILAYANI MPANDA.

Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya nafaka yakiwemo Mahindi na Mpunga Wilayani Mpanda Mkoani Katavi, wamesema kushuka kwa bei ya mazao hayo kumetokana na serikali kuzuia usafirishwaji nje ya nchi.

 Hayo yamebainishwa jana na wafanyabiashara hao wakati wakizungumza na Mpanda radio kuhusu hali ya soko la nafaka kwa sasa Mkoani Katavi.  Mama Sara ni miongoni mwa wafanyabishara wa mazao ya nafaka Wilayani Mpanda ambao wamezungumzia hali hiyo.

  Mama Sara alisema "Bei za mazao zimeshuka  wateja hawapo pia biashara imekuwa ngumu kwani wateja ambao tuliokuwa tunawategemea kununua wamesimama kununua mazao  pia tunaomba serekali kutufungulia mipaka tuweze kuuza mazao yetu nchii za njee ili tuweze kuendesha familia zetu.

 Kwa upande wa wanunuzi akiwemo Bw. Karim Hamis Swalehe pamoja na kuipongeza serikali kukataza kusafirisha mazao nje ya nchi,wamethibitisha bei ya sasa kutofautiana na bei ya miezi mitatu iliyopita. Wamesema bei ya Mahindi imeshuka kutoka 140,000 hadi shilingi 60,000 wakati bei ya Mchele ikishuka kutoka 160,000 hadi Shilingi 130,000 kwa gunia la kilo 100.

 Katika hatua nyingine wamesema kuwa inapofika wakati wa mavuno,wanunuzi hupungua sokoni na hivyo mzunguko kibiashara hudorola. Katika Mkoa wa Katavi,baadhi ya maeneo yanayotajwa kwa kilimo cha mazao ya nafaka hususani Mahindi na Mpunga kwa kiasi kikubwa ni pamoja na Kata za Mwakmulu,Kakese na Iteka katika Wilaya ya Mpanda,Majimoto,Usevya na Mpimbwe Wilayani Mlele na vijiji vya Mwese,Sibwesa na Katuma Wilayani Tanganyika.
 Kauli ya kutosafirishwa kwa nafaka nje ya nchi ilitolewa wiki iliyopita na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa akiwa Mkoani Kilimanjaro.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...