Sunday, 2 July 2017

Wallace Karia akabidhiwa nafasi ya Malinzi

                      Mwemyekiti wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Revocatus Kuuli ametangaza kusimamisha mchakato wa uchaguzi wa shirikisho hilo hadi matatizo yaliyojitokeza yatakaposhughulikiwa.
Kuuli ametangaza kusimamishwa kwa uchaguzi huo alipokutana na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, baada ya kamati hiyo kushindwa kufikia muafaka wa kupitisha majina ya wagombea hasa katika nafasi ya urais.
 Mwenyekiti huyo amesema alilazimika kuiandikia sekretarieti ya TFF barua kuitaarifu kukwama kwa baadhi ya mambo katika mchakato huo na kupendekeza kusimamishwa kwa mchakato, na kisha sekretaieti imemjibu ikiridhia uamuzi huo wa kusimamisha uchaguzi.  
Kuuli ameeleza kusikitishwa kwake na jinsi kamati hiyo inavyolazimisha kufanya kazi zake bila kufuata kanuni na taratibu, kiasi cha kulazimisha baadhi ya wagombea wapitishwe bila kufanyiwa usaili wa ana kwa ana.
Jambo lingine ambalo Kuuli amelitaja kuwa ni kikwazo katika kamati hiyo, ni kitendo cha majina ya baadhi ya wagombea kukatwa bila utaratibu wala kuangalia sifa zao.
Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji (TFF) imepanga kukutana siku ya Jumanne Julai 4 mwaka huu kwa dharura kwa ajili ya kuujadili mchakato huo.
Pia
Kamati ya utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania TFF, imempitisha Wallace Karia kukaimu nafasi ya RAIS wa shirikisho hilo.
Pia kamati hiyo iliyokutana jana, imemteua Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF kuwa Kaimu Karibu Mkuu wa shirikisho hilo.
Viongozi hao watakaimu nafasi hizo mpaka mahakama itakavyoamua vinginevyo kuhusu kesi zinazowakabili viongozi wa sasa ambao ni Rais Jamal Malinzi na Karibu Mkuu Celestine Mwesigwa.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...