Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), imetangaza majina ya wagombea 11 ya waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu mkoani Morogoro.
Majina ambayo yamepitishwa ni Amina Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng'itu, Theresia Mung'ong'o, Hilda Masanche, Salma Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmin Soudy na Chichi Mwidege.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
No comments:
Post a Comment