Shirika la habari la AP linasema kuwa takriban watu 250 wameuawa.
Eneo moja la milima liliporomoka mapema leo Jumatatu kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi kufukiwa.
Mwandishi wa habari aliye eneo hilo anasema kuwa watu wemgi walipatwa wakiwa bado wamelala wakati maporomoko yalitokea
"Mke wangu amekufa, watoto wangu wote wamekufa, Leo asubuhi niliongea na watoto wangu kabla ya kuenda kazini. Mmoja wao hata alinipa soksi nilizovaa." alisema mwathiriwa mmoja.
"Tulikuwa ndani, tukaskjia udongo ukikaribia, tukajaribu kukimbia, nilijaribu kumchukua mtoto wangu, lakini udongo ulikuja kwa haraka sana . Alifukiwa akiwa hai. Sijamuona mume wangu. Mtoto wangu alikuwa na umri wa wiki saba." alisema muathiriwa mwingine.
Maafisa wanasema kuwa ni mapema sana kutoa idadi kamili ya watu waliouawa
Watu wamesambaza picha za uharibifu uliotokea kwenye mtandao wa twitter ya za mafuriko ndani nanje ya mji wa Free town.
Kwa muhimu wa bbcswailI.
No comments:
Post a Comment