Thursday, 23 November 2017

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda mkoani katavi Willium Mbogo amesema stendi kuu ya mabasi ya kisasa inatarajiwa kuanza kufanya kazi


 

Mhe. Willium Mbogo



 Na Rebecca Kija.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Mpanda mkoani katavi Willium Mbogo amesema stendi kuu ya mabasi ya kisasa inatarajiwa kuanza kufanya kazi mwanzoni wa mwaka 2018.

Amebainisha hayo wakati wakizungumza na Mpanda redio kupitia kipindi cha kumekucha Tanzania ambapo amesema hatua iliyobaki ni ujenzi wa vibanda na kukamilisha huduma ya maji na umeme.

Aidha amesema stendi hiyo itakuwa na uwezo wa kuingiza mabasi 60 kwa wakati mmoja  ambapo ametoa wito kwa wamiliki wote wa mabasi kununua mabasi yanayoenda na hadhi ya stendi.

Mkoa wa Katavi umefikisha miaka mitano toka kuanzishwa kwake huku ukipiga hatua kubwa ya kimaendeleo ukilinganisha na mikoa mingine michanga.



No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...