Sunday, 24 September 2017

Kiongozi wa mwenge agomea mradi wa shule

Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour


Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru, Amour Hamad Amour amegoma kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Shule ya Msingi Mkundi ya Mbaru na kuagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza kwa nini imejengwa chini ya kiwango.
Amour alimuagiza Mkuu wa Takukuru wilayani Lushoto, Zozima John kwenda kufanya tathmini ya ujenzi huo ili kujua thamani ya fedha na ubora wa mradi ambao umebainika kuwa na ufa kwenye ukuta, mabati kuezekwa chini ya kiwango na udogo wa vyumba vya madarasa kutokandikwa vizuri.
Alisema ujenzi huo umetumia zaidi ya Sh7 milioni kati ya Sh 11 milioni zinazohitajika kuumalizia.
“Mkurugenzi (wa Halmashauri ya Lushoto, Kazimbaya Makwega) sitaweka jiwe la msingi la mradi huu kwa vile upo chini ya kiwango. Mabati yanatakiwa yawe na ubora wa geji 28, lakini ninyi mmeweka geji 32. Pia, jengo hili limetoa ufa kabla ya kuanza kutumika huku darasa likiwa na vipimo vidogo,” alisema Amour.
Mkuu wa Takukuru, John alisema mradi huo umetekelezwa chini ya viwango ili kuwahi mbio za mwenge na kuongeza hata mabati ya darasa hilo yameezekwa Sept 21, mwaka huu.
Akizungumza juzi baada ya kuupokea mwenge katika Kijiji cha Mkomazi, Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella alisema miradi yote itakayozinduliwa imehusisha nguvu za wananchi, halmashauri, Serikali kuu na wahisani.

@habari na mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...