WATANZANIA wameaswa kuilinda na
kudumisha amani iliyopo nchini na kamwe wasithubutu kushawishiwa na watu
kuivuruga kwa namna yeyote ile.
Kauli hiyo imetolewa na Shehe na
Kadhi mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mustapha Shaaban wakati akitoa mawaidha baada ya
swala ya Eid El Hajj iliyoswaliwa kimkoa katika Msikiti Mkuu wa Gaddafi mjini
Dodoma jana. Shehe Shaaban alisema Tanzania kama mataifa mengi ya afrika
yaliasisiwa na viongozi wetu kwa njia ya amani lakini hadi sasa mataifa mengi
yameshavuruga amani yao na wanaishi maisha ya mashaka, hivyo alisema Watanzania
hawanabudi kujivunia hali ya amani iliyopo pasipo kuivuruga.
“Urithi wetu ni amani na utulivu nan
i urithi wa umma wa waislamu dunia nzima hivyo hatuna budi kuendeleza na
kudumisha upendo, amani na mashikamano katika familia zetu, jamii na hata kwa
taifa kwa ujumla, kama ambavyo Mtume wetu, Muhamad (S.AW) alituhusia kufanya
katika swala yake ya mwisho ya Hijja,” alisema Shehe Shaaban.
Aidha alisema amani ya nchi yetu na
Afrika ni amani yenye historia kutoka kwa waasisi wa mataifa yetu akiwataja,
Mwl. Julius Nyerere, Nelson Mandela, Kwame Nkruma, Mohamad Gaddafi, Jomo
Kenyatta na wengine wengi.
Akitolea mfano wan chi ya Libya,
Shehe Shaaban, alisema taifa hilo lilikuwa ni lenye amani na utajiri mkubwa
Afrika lakini kutokana na kukubali chokochoko toka mataifa mengine waliamua
kuvuruga amani yao na sasa wapo katika hali mbaya ya kiuchumi.
Katika hatua nyingine, Shehe Shaaban
amewaasa wakazui wa mkoa wa Dodoma kutitumia fursa ya ujio wa serikali na
viongozi wake mjini Dodoma katika kujipatia maendeleo. Alisema Maendeleo ya
wana Dodoma hayanabudi kuletwa na wenyeji wenyewe kwanza na wasisubiri wageni
ndio walete maendeleo. Alizitaka taasisi za dini, mashirika na taasisi
mbalimbali za mkoani Dodoma kuwekeza katika maeneo mbalimbali yakiwepo ya elimu
na viwanda ili kuleta maendeleo..
@habari toka mwananchii
No comments:
Post a Comment