Jiwe kubwa
zaidi kuwahi kupita karibu na dunia katika kipindi cha karibu karne moja
linatarajiwa kupita karibu na sayari ya dunia umbali wa karibu maili milioni
4.4 , kimesema kituo cha masuala ya anga za juu cha Marekani, Nasa.
Vipimo vya Florence vilikadiria
umbali wa maili 2.7 sawa na kipenyo cha 4.4 na kwamba jiwe hilo halina tisho
kwa dunia kwa karne zijazo
Mawe mengine yaliyowahi kupita
karibu na dunia, yalikadiriwa kuwa ni madogo sana.
Mawe hayo ambayo yana umbo la vifusi
upande wa kushoto ni masalia yaliyobaki wakati wakuundwa kwa jua na sayari.
Jiwe la Florence - lililogundulika
mnamo mwaka 1981- linaweza kuwa mara 18 ya wastani wa umbali baina ya dunia na
mwezi.
"Florence ni jiwe kubwa zaidi
kuwahi kupita karibu na dunia yetu tangu kuanzishwa kwa mpango wa shirika la
anga za mbali la Marekani NASA wa kuchunguza na kubaini mawe yaliyopo karibu na
dunia ," Amesema Paul Chodas, meneja wa kituo cha NASA kinachochunguza
vitu vilivyopo karibu na dunia katika taarifa yake.
Ugunduzi wa mwaka 2017 ni wa jiwe la
angani lililopo karibu tangu mwaka 1890 na ukaribu huo hautawahi kutokea hadi
baada miaka 2500, shirika la masuala ya anga la Marekani limeongeza.
Mpango wa wanasayansi kuchunguza
ukaribu wa jiwe, kwa kutumia mtambo wa rada wa ardhini unafanyika California na
Puerto Rico.
Wataalam wa anga za juu pia watakuwa
wakilichunguza jiwe hilo yamesema majarida ya masuala ya anga ya Sky na
Telescope.
Jiwe ni rahisi kuliona kwa kutumia
kifaa cha uchunguzi , si kwa sababu tu ni kubwa , lakini pia kwa sababu huakisi
20% ya mwanga wa jua ambao huchoma kwenye sehemu yake ya chini.
Kinyume chake mwezi huakisi wastani
wa 12% pekee.
Kitu chenye ukubwa wa
Florencekinaweza kuwa na athari ya kugonga dunia. Wanasayansi wanaamini kuwa
sasa wamebaini zaidi ya 90% ya miamba ya aina hiyo ya kutisha inayopita angani
karibu na sayari yetu.
#habari toka Bbc swahili
No comments:
Post a Comment