Vikundi vya polisi jamii na ulinzi shirikishi katika
kata ya Misunkumilo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi vimeanza kushiriki katika
ulinzi na usalama baada ya kusitisha kwa muda mrefu.
Hatua
hiyo imethibitishwa na Afisa mtendaji wa kata ya Misunkumilo Bw.Januari
Kayungilo katika Mazungumzo maalumu na Mpanda Radio kuhusu namna wanavyoendesha
ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Awali
Kamanda wa jeshi la polisi Mkoani Katavi ACP Damas Nyanda alikuwa ameiambia
Mpanda Radio kuwa hana taarifa za polisi kutoshiriki ulinzi na usalama katika
kata ya misunkumilo nyakati za usiku ambapo amelazimika kuingilia kati na
hatimaye kuitishwa mkutano ambao umerejesha ushirikiano kati ya Polisi,wananchi
na viongozi.
Kata
ya Misunkumilo yenye mitaa ya Misunkumilo,Mtemi Beda,Kampuni na kijiji cha
Milala ina wakazi zaidi ya Elfu kumi.
No comments:
Post a Comment