KIGOMA.
WAKULIMA zaidi ya 350
katika kata ya Nguruka wilaya ya Uvinza Mkoa wa Kigoma wanatarajia kunufaika
kwa kujiongezea kipato chao kupitia kilimo cha zao la Korosho.
Hatua hiyo imetokana na
ombi la wakulima kuiomba serikali iweze kuwabadilishia zao mbadala la
kibiashara ambapo taasisi ya utafiti
NALIENDELI ilifanya utafiti na
kudhibitisha kuwa zao hilo la Korosho linaweza kulimwa katika wilaya hiyo
kutokana na rutuba iliyopo.
Wakizungumiza mataraji
yao Ahmadi Habibu na juma kyanga ambao ni wakulima waliopatiwa mafunzo hayo wamesema
yatawasaidia kujikwamua zaidi.
Zao hilo kwa mkoa wa Kigoma limeanza kulimwa
kwa mara ya kwanza ambapo bodi ya Korosho imetoa tani moja ya mbegu ambazo
zitatoa fursa ya kulima hekari 5000 katika Tarafa ya Nguruka, Huku afisa kilimo wilaya ya uvinza Bw. Daniel Kamwela akiitaja mipango zaidi
katika kuelekea mpango huo wa kulima korosho
Wakulima wa wilaya ya
Uvinza zao lao kuu la kibiashara ni zao la Tumbaku ambapo kutokana na mahitaji
ya kukuza kipato chao waliomba serikali iweze kuwasaidia kupata elimu ya kilimo
cha zao la Korosho wakiamini kuwa ni zao
kuu la kibiashara na linaweza kuwa chachu ya ukuaji wa uchumi wao lakini pia
kwa Taifa.
No comments:
Post a Comment