Friday, 10 November 2017

Mpanda: Bei ya mazao ya chakula nchini imedaiwa kushukaikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka uliopita.


MPANDA
Bei ya mazao ya chakula nchini imedaiwa kushuka ikilinganishwa na kipindi kama hiki mwaka uliopita.

Baadhi ya wafanyabiashara wa nafaka mjini Mpanda wamesema sababu inayochangia kushuka kwa bei ya nafaka kuwa ni pamoja na serikali kupiga marufuku  usafirishaji wa nafaka nje ya nchi huku ikiruhusu nafaka kutoka nje ya nchi kuingizwa nchini

Wafanyabiashara hao wameiomba serikali kuliangalia upya suala hilo kwani wanapata wakati mgumu kuuza mazao waliyoyanunua kwa bei ya juu na sasa wakilazimika kuuza kwa bei ya hasara

Mwezi julai mwaka huu.

 Serikali kupitia kwa waziri mkuu Kassim Majaliwa ilitoa tahimini ya upugufu wa chakula nchini hivyo kupiga marufuku usafirishaji wa chakula nje ya nchi. 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...