Friday, 10 November 2017

Wizara ya Mali asili na Utalii imesema haina mpango wa kuruhusu shughuri za kilimo katika Kijiji cha Matandalani na Igongwe kata ya Stalike


KATAVI

Wizara ya Mali asili na Utalii imesema haina mpango wa kuruhusu shughuri za kilimo katika Kijiji cha Matandalani na Igongwe kata ya Stalike iliyopo mkoani Katavi.

Kauli hiyo imetolewa na naibu Waziri wa Mali asili na Utalii Japhet Hasunga alipo kuwa akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Nsimbo mkoa wa Katavi Richad Mbogo ambaye amehoji kwanini maeneo hayo yasi idhinishwe kisheria kwa shughuri za kibinadam.

Akijibu swali hilo amesema serikali imetenga maeneo mengine kwaajili ya wakazi walio ondolewa katika maeneo hayo yanayo tajwa kuwa hifadhi za misitu.

Katika hatua nyingine amefafanua uwepo wa mpango wa kuyapitia upya maeneo hayo ili kuona uwezekano wa kubadilisha matumizi pale itakapo onyesha ulazima huo.

Mara kwa mara mamia ya wakazi mkoani Katavi wamekuwa wakiondolewa  kinguvu katika maeneo mbali mbali ya vitongoji na Vijiji kwa madai ya kuvamia misitu.


Source :Alinanuswe Edward

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...