Na Issack Gerald
Wanawake wote wajawazito katika
kijiji cha Mtambo kata ya Katumba Wilayani Mpanda Mkoani Katavi,wanalazimika kubeba
maji kutoka nyumbani na kuyapeleka katika zahanati ya Mtambo iliyopo kijijini
hapo ili yatumike wakati wakijifungua.
Mganga mfawidhi wa zahanti hiyo
Dkt.Daud Mashama amesema wanawake wajawazito wasipokuja na maji hulazimika
kufuata maji mto Lutonya uliopo umbali wa kilomita 8 kutoka zahanati ya Mtambo.
Katibu wa kijiji cha Mtambo Bw.Fenias
Fulujensi amesema wanasubiri uwekaji wa mitambo katika kisima kilichochimbwa
huku kaimu Afisa Mtendaji Kata ya Katumba Bi.Lucy Kagine akisema suala hilo linafanyiwa
kazi.
Hivi karibuni wananchi wa Kata ya
Katumba walilalamika kukosa maji ya chanzo cha maji ya Ikorongo wakisema maji
usafirishwa kutoka Katumba mpaka Mpanda Mjini na wao kukosa huduma hiyo licha
ya chanzo hicho kuwa katika kata yao serikali haiwatendei haki.
Juhudi za kuwatafuta uongozi wa
Halmashauri ya wilaya ya Nsimbo kuhusiana na tatizo hilo zinaendelea.
No comments:
Post a Comment