Saturday, 2 September 2017

Wanafunzi 7 wafariki katika moto uliochoma bweni Kenya


Maafisa wa polisi wakishika doria nje ya shule ya Moi Girls liliopo jijini Nairobi nchini Kenya ambapo takriban wanafunzi saba wamefariki baada ya bnweni lao kuchomeka
Image captionMaafisa wa polisi wakishika doria nje ya shule ya Moi Girls liliopo jijini Nairobi nchini Kenya
Wanafunzi saba wamefariki na makumi wengine wakijeruhiwa baada ya moto kuchoma bweni la shule ya Moi Girls mjini Nairobi.
Waziri wa elimu Fred Matiang'i amesema kuwa wanafunzi wengine 10 walijeruhiwa na wamelazwa hospitalini.
Wawili kati ya 10 wako katika hali mbaya ,kulingana na madaktari huku wengine wanane wakiwa hawako katika hali mbaya.
Takriban wanafunzi 10 wamerodheshwa kuwa hawajulikani waliko kulingana na kitengo cha habari cha maafisa wa msalaba mwekundu katika shule hiyo.
Baadhi ya wazazi na wakaazi wa eneo la shule hiyo waliojitokeza kujaribu kuwajulia hali wanawao katika shule hiyo
Image captionBaadhi ya wazazi na wakaazi wa eneo la shule hiyo waliojitokeza kujaribu kuwajulia hali wanawao katika shule hiyo
Matiang'i amesema kuwa shule hiyo imefungwa kwa wiki mbili huku uchunguzi ukianzishwa kuhusiana na sababu ya moto huo.
Waziri huyo hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha nne wataendelea na masomo yao ifikiapo siku ya Ijumaa na watasaidiwa kuendelea na masomo yao wakati ambapo wanajianda kufanya mtihani wa kidato cha nne wa KCSE.
Amesema kuwa kundi la wataalam wa upasuaji ikiwemo madaktari wako katika shule hiyo kubaini chanzo cha moto huo.
Magari ya kukabiliana na dharura yalifilka katika shule hiyo mapema alfajiri ili kuswanusuru walioathirika
Image captionMagari ya kukabiliana na dharura yalifilka katika shule hiyo mapema alfajiri ili kuswanusuru walioathirika
Amesema kuwa mkuu wa shule hiyo amewataka wazazi kuwachukua wanawao.
Bwana Matiang'i aliandamana na gavana wa Nairobi Mike Sonko.
Kulingana na gazeti la Daily Nation nchini humo mwanafunzi mmoja wa kidato cha kwanza ambaye alikuwa miongoni mwa wale waliotibiwa baada ya kisa hicho alisema kuwa moto huo ulianza mwendo wa saa saba usiku.
Baadhi ya wazazi waliofika katika shule hiyo kuwachukua wana wao
Image captionBaadhi ya wazazi waliofika katika shule hiyo kuwachukua wana wao
Alisema kuwa bweni lililochomeka lilikuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza na kwamba kulikuwa na makelele ya wanafunzi waliojaribu kujinusuru mbalii na mkanyagano huku wasichana wakijaribu kutoka ndani ya bweni hilo.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...