Moja ya sababu za kuhojiwa kwake ni kutamka kwamba
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa na wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga
“ni wajinga na wapumbavu” kutokana na kufanya matendo ambayo ni kinyume na
ubinadamu ambayo yanamvunjia heshma Rais John Magufuli aliyewateua.
Mbunge
wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema jana alihojiwa na polisi kwa zaidi ya
saa tatu, kutokana na kauli alizotoa kwenye mikutano ya hadhara iliyomalizika
hivi karibuni.
Moja
ya sababu za kuhojiwa kwake ni kutamka kwamba Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius
Byakanwa na wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga “ni wajinga na wapumbavu”
kutokana na kufanya matendo ambayo ni kinyume na ubinadamu ambayo yanamvunjia
heshma Rais John Magufuli aliyewateua.
Lema
alikuwa kituo kikuu cha polisi cha Arusha kuanzia saa 7:14 mchana hadi saa
10:00 jioni kwa mahojiano katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO).
Akizungumza
na waandishi wa habari mara baada ya kuachiwa kwa dhamana hadi Septemba 19,
Lema alisema ni kweli kitendo alichofanya mkuu huyo wa wilaya ya Hai cha
kumuweka rumande mwalimu aliyeshindwa kumtaja jina lake, ni cha udhalilishaji
na hakiendani na hadhi ya mkuu wa wilaya.
Lema
pia alisema kitendo cha mkuu mwingine wa wilaya ya Chemba, Odunga kumchapa
viboko mzazi ambaye mtoto wake alirusha jiwe kwenye gari, ni cha ajabu na
udhalilishaji mkubwa na hakuna jina jingine la kumuita zaidi ya “mjinga”.
“Nimewaeleza
polisi ni kweli nilisema na nikawaambia nina imani na Rais John Magufuli kuwa
hataendelea kuwaacha salama wakuu hawa wa wilaya hizo kwa kuwa walifanya
matendo ambayo ni ya kipumbavu na kijinga licha ya kuomba msamaha,” alisema mbunge
huyo anayeongoza Jimbo la Arusha Mjini kwa kipindi cha pili.
Lema
alisema anakumbuka alimshauri Rais katioka mikutano yake awachukulie hatua
viongozi hao kwa kuwa wanafifisha jitihada zake.
“Matendo
haya ni ya kinyama na udhalilishaji na hayana lugha nyingine ya kuyakemea zaidi
ya kuyaita ni ya kipumbavu na kijinga,” alisema.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo hakupatikana jana kueleza sakata hilo.
Hata
hivyo, ofisa mmoja wa polisi mkoani hapa alithibitisha kuhojiwa kwa Lema na
kueleza kuwa ameachiwa kwa dhamana ya polisi kwa kuwa uchunguzi unaendelea.
No comments:
Post a Comment