Thursday, 28 September 2017

Waziri, wabunge 25 wasimamishwa kuhudhuria vikao Uganda.


Spika wa Bunge la Uganda Rebecca Kadaga amewasimamisha waziri mmoja na wabunge 25 kuhudhuria vikao vya bunge kwa madai ya kushiriki katika vurugu ambayo ilimlazimisha kuahirisha kikao siku ya Jumatano.
Mmoja wa waliozuiliwa kuhudhuria vikao ni Waziri wa Maji, Ronald Kibuule kwa madai ya kwenda katika ukumbi wa bunge akiwa na silaha.
Wabunge wengine waliosimamishwa kuhudhuria kikao wengi wao ni wa upinzani wanaopinga kufutwa kwa kifungu 102(b) kutoka katika katiba ambayo inakataza watu ambao wanaumri zaidi ya miaka 75 kugombea nafasi ya urais, ambao wamekataa kutoka katika ukumbi wa bunge na kumlazimisha spika kuahirisha kikao.
Wale waliozuiwa kuhudhuria vikao vya bunge ni : Robert Kyagulanyi aka Bobi Wine (Kyaddondo Mashariki), MP Allan Ssewanyana (Makindye Magharibi),Monica Amoding (Wilaya ya Kumi ), Dr Sam Lyomoki (Wafanyakazi) Betty Nambooze (Manispaa ya Mukono) Ibrahim Kasozi (Makindye Mashariki) andMoses Kasibante (Rubaga Magharibi).
Baada ya mgogoro huo, maafisa wa ulinzi wakiwa katika vazi la suti walivamia Ukumbi huo na kuwalazimisha Kyagulanya na Ssewanyana kutoka nje.
Serikali ya Uganda inataka kuondoa ukomo wa umri kwa wagombea urais kitu kilicholeta vurugu Jumatano katika bunge la Uganda.
Hatua hivyo ya serikali itamwezesha Yoweri Museveni kuendelea na nafasi yake ya urais.
Sheria hizo zilikuwa tayari zimebadilishwa 2005 zikiondoa ukomo wa awamu mbili ambapo ilimwezesha Museveni ambaye sasa ana umri wa miaka 72 na awamu yake ya tano, kuendelea kuwepo katika madaraka.
Chini ya katiba iliyokuwepo Rais Museveni atakuwa amepitiliza umri unaoruhusiwa na katiba kugombea katika uchaguzi wa mwaka 2021.
@habari na voa swahili

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...