Mmoja wa watoto katika eneo la Afrika mashariki |
Zaidi ya watoto 800,000 wako katika hatari ya kukumbwa na njaa huko Afrika mashariki na mashirika ya misaada yana wiki kadhaa tu kuwaokoa. Shirika la hisani la World Vision limesema Jumatano.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters mzozo nchini Sudan Kusini na ukame wa muda mrefu ambao umelikumba eneo hilo umewaacha zaidi ya watoto milioni 15 wakiwa na shida ya chakula, maji, huduma za afya, elimu au ulinzi imesema idara ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto- UNICEF.
Nchi ya Ethiopia, Somalia na Kenya zimeshuhudia kupanda kwa viwango vya njaa miongoni mwa watoto katika wiki za karibuni huku maeneo kadhaa yakiripoti zaidi ya theluthi moja ya watoto wana matatizo ya afya ikiwa ni matokeo ya hali hiyo taarifa ya World Vision ilisema. “Bado tuko katika hali ya hatari zaidi ya watoto 800,000 wana utapiamlo uliokithiri na wako katika hatari ya kukumbwa na njaa ambayo itapelekea vifo alisema Christopher Hoffman mkurugenzi wa Afrika mashariki wa World Vision. Tuna wiki chache tu kusitisha hali hii kutokea”.
@habari na VOA swahili
No comments:
Post a Comment