Rais wa Tanzania Dkt. john magufuli |
RAIS John Magufuli amefanya uteuzi wa makatibu wakuu wapya pamoja, naibu makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na mabalozi wawili akiwamo aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Inspekta Jenerali Ernest Mangu.
Mbali ya IGP Mangu, Rais Magufuli pia amemteua aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Aziz Mlima kuwa Balozi ambaye pamoja na Mangu watapangiwa vituo vya kazi.
Mei 28, mwaka huu, Rais Magufuli alitengua uteuzi wa IGP Mangu na kumteua aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro kuongoza Jeshi la Polisi. Katika uteuzi uliotangazwa jana jioni na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi, umeshuhudia wakuu wa wilaya wanne wakipanda na kuwa wakuu wa mikoa.
Balozi Kijazi aliwataja waliopandishwa kuwa wakuu wa mikoa na mikoa yao katika mabano ni waliokuwa wakuu wa wilaya za Dodoma Mjini, Christine Mndeme (Dodoma), Korogwe - Robert Gabriel (Geita), Arumeru – Alexander Mnyeti (Manyara) na Nanyumbu – Joachim Wangabo (Rukwa) na Hai - Gelasius Byakanwa (Mtwara).
Alipokuwa ziarani mkoani Tanga miezi michache iliyopita, Rais Magufuli alivutiwa na utendaji wa DC Gabriel na kueleza kwamba kwa uchapakazi huo, haitashangaza kama aatapewa nafasi ya juu zaidi huku wananchi wa Korogwe wakiomba kwa rais asimuondoe wilayani humo.
Katika uteuzi huo wa wakuu wa mikoa, Rais John Magufuli pia amemteua aliyekuwa Naibu Waziri katika Serikali ya Awamu ya Nne, Adam Malima kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara akichukua nafasi ya Dk Charles Mlingwa ambaye kama Dk Joel Bendera (Manyara), Zelothe Stephen (Rukwa) na Ezekiel Kyunga (Geita) kustaafu.
Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana hawakuteuliwa. Kwa upande wa makatibu wakuu na manaibu katibu wakuu, Balozi Kijazi alisema Rais Magufuli amefanya uteuzi wa manaibu katibu wapya saba na kuwapandisha wanne.
Wateule wote hao wataapishwa Ikulu leo saa 8 mchana. Wakuu wa mikoa Kwa upande wa wakuu wa mikoa ni Manyara - Alexander Mnyeti (alikuwa DC Arumeru); Rukwa - Joachim Wangabo (DC Nanyumbu); Geita - Robert Gabriel Lughumbi (DC Korogwe); Mara - Adam Malima (alikuwa Naibu Waziri Awamu ya Nne); Dodoma - Christine Mndeme (DC Dodoma Mjini) na Mtwara - Gelasius Byakanwa (DC wa Hai).
Uteuzi wa Mabalozi
Dk Aziz Mlima - amekuwa Balozi (alikuwa Katibu Mkuu Mambo ya Nje), na IGP mstaafu Ernest Mangu. Vituo vyao vya kazi vitatangazwa baadaye.
Uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu wao
Ofisi ya Rais Ikulu - Katibu Mkuu Alphayo Kidata; Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora - Katibu Mkuu, Dk Laurean Ndumbaro, Naibu Katibu Mkuu orothy Mwaluko; Ofisi ya Rais TAMISEMI - Katibu Mkuu Mussa Iyombe, Naibu Katibu Mkuu (Afya) - Zainabu Chaula na Naibu Katibu Mkuu (Elimu) – Tixon Nzunda.
Ofisi ya Makamu wa Rais - Katibu Mkuu, Joseph Manongo (alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo), Naibu Katibu Mkuu -Butamo Philipo; Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi na Ajira - Katibu Mkuu Erick Shitindi; Bunge na Waziri Mkuu - Katibu Mkuu Maimuna Tarishi na Sera - Katibu Mkuu Profesa Faustine Kamuzora (amehamishwa kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais).
Wizara ya Kilimo - Katibu Mkuu Mathew Mtigumwe na Naibu Katibu Mkuu – Dk Thomas Kashilillah aliyekuwa Katibu wa Bunge; Wizara ya Mifugo na Uvuvi - Mifugo - Katibu Mkuu, Dk Maria Mashingo na Uvuvi - Katibu Mkuu, Dk Yohana Budeba.
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano- Uchukuzi - Katibu Mkuu Dk Leonard Chamuriho, Ujenzi - Katibu Mkuu Joseph Nyamhanga, Mawasiliano - Katibu Mkuu Dk Maria Msasabo na Naibu Katibu Mkuu Mawasiliano Adelina Madete.
Wizara ya Fedha na Mipango - Katibu Mkuu Dotto James Mgosha, Naibu Katibu Mkuu Utawala Suzan Mkapa, Naibu Katibu Mkuu Fedha za Nje Amina Shaaban na Naibu Katibu Mkuu Sera - Dk Hakingu Kazungu.
Wizara ya Nishati - Katibu Mkuu Dk Hamis Mwinyimvua (alikuwa Ofisi ya Waziri Mkuu) wakati Wizara ya Madini - Katibu Mkuu Profesa Simon Msanjila (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu), wakati Wizara ya Katiba na Sheria - Katibu Mkuu Profesa Sifuni Mchome na Naibu Katibu Mkuu - Amon Mpanju (wote wanaendelea hapo).
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki - Katibu Mkuu Profesa Adolf Mkenda (ambaye ni mchumi, anatoka Wizara ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji) Naibu Katibu Mkuu - Balozi Ramadhan Muomba Mwinyi (anaendelea) na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa - Katibu Mkuu Dk Florens Turuka na Naibu Katibu Mkuu Emmaculate Ngwale.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Projest Rwegasira, Wizara ya Maliasili na Utalii Katibu Mkuu Gaudence Milanzi na Naibu Katibu Mkuu Aloyce Nziku, Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji, Profesa Elisante Ole Gabriel (anatoka Habari), manaibu wake ni Ludovick Mayeye (Viwanda) na Joseph Rushaija; Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ni Profesa Mpoki Ulisubya (Afya na Sihaba Nkinga (Maendeleo ya Jamii).
Wizara ya Elimu, Teknolojia na Ufundi - Katibu Mkuu Leonard Akwilapo na manaibu Profesa Ephifani Mdoe (alikuwa Naibu Nishati na Madini) na Dk Eva-Maria Semakafu; Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi- Katibu Mkuu Dorothy Mwanyika (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Fedha) na Naibu Katibu Mkuu ni Moses Kusiluka.
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Katibu Mkuu ni Suzan Mlawi (alikuwa Naibu Katibu Mkuu Utumishi) na Naibu Katibu Mkuu ni Nicholaus William wakati Wizara ya Maji na Umwagiliaji Katibu Mkuu ni Profesa Kitila Mkumbo na Naibu Katibu Mkuu Emmanuel Kalobelo.
@habari toka habari leo
No comments:
Post a Comment