Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Suleman Jafo |
DAR ES SALAAM
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh.Suleman Jafo,amewaagiza wakurugenzi
watendaji wa Halmashauri nchini, kuwasilisha michango ya watumishi katika
mifuko ya hifadhi ya jamii.
Waziri Jafo ametoa kauli hiyo leo
alipokuwa akihojiwa na kituo cha runinga cha cloud kufuatia malalamiko kutoka
kwa baadhi ya watumishi hapa nchini wakiwemo walimu wakilalamika kutopata mafao
yao kwa wakati wanapostaafu.
Hata hivyo siyo mara ya kwanza
serikali kuagiza mafao ya watumishi yawasilishwe katika mifuko ya hifadhi ya
jamii suala ambalo waziri Jafo amesema kama ulikuwa ni uzembe wa waajiri
hautaendelea wala kuvumiliwa.
@habari na clouds tv
No comments:
Post a Comment