Tuesday, 24 October 2017

Serikali yaifutia TTCL deni la Sh76 bilioni.


Dar es Salaam. 
Wakati kampuni zote zikitakiwa kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE), Serikali imeifutia deni la Sh76 bilioni Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kuligeuza mtaji ili iweze kuimarisha uwezo na kutekeleza majukumu yake kwa ushindani.
Kwa mamlaka aliyonayo chini ya kifungu cha 5(3) na 9 cha Sheria ya Fedha, Waziri wa fedha na mipango, Dk Philip Mpango alibadilisha deni hilo kuwa mtaji Agosti.
Taarifa iliyotolewa na Msajili wa Hazina, Dk Oswald Mashindano inasema lengo la kugeuza mkopo huo kuwa mtaji ni kuitaka TTCL kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, tija na weledi ili kuongeza ushindani katika soko.
Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) ya mwaka 2010 inazitaka kampuni zote za mawasiliano kujiorodhesha DSE. Mwisho wa kufanya hivyo ilikuwa Juni, lakini ni Vodacom pekee iliyokamilisha agizo hilo huku nyingine zikiwa bado.
@habari na mwananchi

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...