Tuesday, 28 November 2017

Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe


Bw Robert  Mugabe


 

Serikali ya Zimbabwe imetangaza siku kuu mpya ya kukumbuka mchango wa Robert Mugabe ambaye aliondolewa madarakani wiki iliyopita.

Gazeti la serikali la Herald limesema sikukuu hiyo itakuwa ikiadhimishwa siku ya kuzaliwa kwa Bw Mugabe kila mwaka.

Serikali ya Bw Mugabe ilikuwa imeamua kutangaza siku ya kuzaliwa kwake kuwa sikukuu ya taifa mwezi Agosti, baada ya kampeni kutoka kwa mrengo wa vijana katika chama cha Zanu-PF.

Bw Mnangagwa, makamu wa rais aliyekuwa amefutwa kazi wiki iliyotangulia na kutorokea nje ya nchi, akarejea na kuchukua usukani na kuapishwa Ijumaa baada ya Bw Mugabe kushurutishwa kujiuzulu.

CHANZO: DW KISWAHILI.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...