Saturday, 25 November 2017

Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoiogopa mahakama.





Na Alinanuswe Edward.

Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutoiogopa mahakama kwa kuwa ipo kwa ajili ya kushughulikia mahitaji ya wananchi katika kupatikana na kwa haki zao.

Wito huo umetolewa na hakimu mwandamizi wa mahakama ya mwanzo mjini Mpanda Mh.David Daniel Mbembela kupitia kipindi cha kumekucha Tanzania kinachorushwa cha Mpanda Radio.

Aidha amewashauri wananchi kujenga tabia ya kufika katika mahakama kwa ajili ya kujifunza namna kesi zinavyoendeshwa mahakamani.

Wakati huo huo Mh.Mbembela amesema serikali imeleta baraza la ardhi la wilaya mkoani Katavi kwa ajili ya kusikiliza migogoro na kesi zinazohusu masuala ya ardhi ambapo awali wakazi wa Mkoa wa Katavi walikuwa wakipata huduma hiyo wilayani Sumbawanga Rukwa.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...