Monday, 27 November 2017

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku kufanyika maandamano wiki hii ya kupinga kuendelea kuwepo madarakani kwa Rais Joseph Kabila



 

Kiongozi wa upinzani Felix Tshishekedi wa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo

Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imepiga marufuku kufanyika maandamano wiki hii ya kupinga kuendelea kuwepo madarakani kwa Rais Joseph Kabila.

Taarifa iliyochapishwa katika mitandao ya habari nchini Congo imesema maafisa katika mji mkuu Kinshasa wamepiga marufuku maandamano yote yaliyokuwa yamepangwa wiki hii.

Wafuasi wa Rais Kabila walikuwa wamepanga maandamano kesho Jumanne kuunga mkono kucheleweshwa kwa chaguzi hadi Desemba mwaka ujao.

Awali, upinzani pia ulikuwa umepanga maandamano kumpinga Kabila hapo kesho lakini ikaahirisha hadi Alhamisi.

Kiongozi wa upinzani Felix Tshishekedi amesema atapuuza marufuku hiyo na kuwataka Wacongo kujitokeza kwa wingi kuandamana tarehe 30 mwezi huu.

CHANZO: DW KISWAHILI.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...