WAZIRI Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa |
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa
amemuagiza Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera kufanya ukaguzi
na kuyaondoa mara moja maduka ya dawa za binadamu yaliyopo jirani na zahanati,
vituo vya afya na hospitali za serikali.
Hii ni mara ya pili katika
kipindi cha mwaka mmoja Waziri mkuu kutoa agizo hilo na kuwaagiza wakuu wa
wilaya na wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya, miji na manispaa
mkoani Ruvuma kuyaondoa kwa nguvu maduka yote ya dawa za binadamu jirani na
hospitali za umma.
Amesema kuwa kuwepo maduka
hayo jirani kunaweza kuwaaminisha wananchi kwamba hata dawa zilizopo katika
maduka hayo zinatoka katika hospitali za serikali, kwa hiyo ni vema wahusika
wakazingatia agizo hilo ili kuepusha malalamiko ya wananchi.
No comments:
Post a Comment