TAARIFA kutoka vituo
mbalimbali vya afya vilivyopo katika Manispaa ya Mpanda zinaonesha kuwa
wasichana wapatao 624 wenye umri chini ya miaka 18 wamejifungua katika vituo
vinavyotoa huduma za afya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Meja
Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga, ameyasema hayo katika uzinduzi wa Kampeni ya
Siku 16 za Kupinga Ukatili wa Kijinsia uliofanyika kimkoa katika Viwanja vya
Saba Saba, katika Kijiji cha Kabungu wilayani Tanganyika.
Muhuga yeye amesema, Utafiti
wa Afya ya Uzazi na Mtoto na Viashiria vya Malaria wa 2015 na 2016 uliofanywa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, unaonesha Mkoa wa Katavi unaongoza
kitaifa kwa mimba za utotoni.
Aidha amesema ilibainika
kuwa, asilimia 45 ya wasichana wenye umri wa miaka kati ya 15 na 19 wameshazaa
huku asilimia 33.3 wakiwa na mtoto aliye hai angalau mmoja
Hata hivyo amesema kuwa mashauri
401 ya ukatili yalihusu ukatili wa kimwili, 66 kingono, 262 kisaikolojia na 447
yalihusu kutelekeza watoto na familia zao
na ukatili wa kimwili na kingono ulifanywa na wanaume.
No comments:
Post a Comment