Monday, 27 November 2017

Diwani wa kata ya Misunkumilo iliyopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Bwana Matonda Alfred amesema kata hiyo imefanikiwa kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.

 

Na Haruna Juma 

Diwani wa kata ya Misunkumilo iliyopo manispaa ya Mpanda mkoani Katavi Bwana Matonda Alfred amesema kata hiyo imefanikiwa kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja mbalimbali.

Bw. Matonda amesema katika bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18 kata hiyo imefanikiwa na inaendelea na utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika sekta ya afya, elimu, maji na miundombinu

Katika hatua nyingine amesema kata hiyo inakabiliwa na changamoto ya ongezeko la watu katika kata hiyo hasa katika kijiji cha Milupwa lakini hilo haliwezi kuathiri juhudi mbali mbali zinafonywa na viongozi  kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo

Aidha amewaomba wananchi wa kata hiyo kuendelea kuchangia miadi ya maendeleo pale wanapoombwa kufanya hivyo na kuunga mkono uongozi uliopo madarakani ili kuharakisha juhudi za kuwaletea maendeleo.


No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...