Tuesday, 5 December 2017

Chama cha Walimu mkoa wa katavi CWT kinakusudia kuchukua hatua zaidi kutokana na fedha za walimu manispaa ya Mpanda za makato katika mfuko wa Jamii PSPF kwa 2008 kutofikishwa.


KATAVI
Chama cha Walimu mkoa wa katavi CWT kinakusudia kuchukua hatua zaidi kutokana na fedha za walimu  manispaa ya Mpanda za makato katika mfuko wa Jamii PSPF kwa  2008 kutofikishwa.

Hayo yamesemwa na Katibu wa chama cha walimu mkoa wa Katavi Hamisi Chinahova alipozungumza na Mpnda radio mapema ambapo amesema suala hilo halijapatiwa ufumbuzi mpaka sasa.

Katika hatua nyingine amelitaja suala la kukithiri kwa madai mbali mbali ya walimu kuwa kikwazo katika utendaji kazi ikiwemo kufikia Malengo ya kitaifa.

Mwaka 2015 yaliibuka madai haya na kupelekea baadhi ya walimu kufanya maandamano ya amani mpaka ofisi ya mkuu wa mkoa ili kushinikiza malipo ya madeni zikiwemo stahiki mbali mbali.


SOURCE:ALINANUSWE

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...