Tuesday, 5 December 2017

Wiki chache baada ya Mpanda Radio kuripoti matukio ya ajali katika makutano ya barabara ya Kigoma na Sumbawanga eneo la Super City kwa kukosekana kwa alama za usalama barabarani serikali imeanza kuchukua hatua.

MPANDA

Hatua hizo ni pamoja na kuanza kwa uwekaji wa alama mbalimbali pamoja na ujenzi wa eneo la mzunguko utakaowasaidia watuamiaji wa barabara kupita kwa mfumo bora ukilinganisha na awali.

Mpanda Radio imezungumza na baadhi ya watumiaji wa barabara hizo ambapo wameishukuru serikali kwa hatua hizo na kukiri kupungua kwa ajali katika eneo hilo.

Hapo awali eneo la Super City kuliripotiwa kutokea kwa ajali kadhaa zilizosababisha vifo na majeruhi.

SOURCE: MDAKI HUSSEIN

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...