Tuesday, 5 December 2017

Watu wenye ulemavu Mkoani Katavi,wameeleza kusikitishwa na kauli ya serikali kuwa haina pesa za kuwawezesha kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.


KATAVI

Watu wenye ulemavu Mkoani Katavi,wameeleza kusikitishwa na kauli ya serikali kuwa haina pesa za kuwawezesha kufanya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.

Kauli hiyo wameitoa  katika kikao cha kupanga tarehe nyingine ya maadhimisho ambapo wamepanga yafanyike Desemba 19 mwaka huu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA Mkoani Katavi Issack Mlela amesema serikali kutowawezesha kufanya maadhimisho ni kutowatendea haki wakati serikali inasema mapato yameongezeka serikalini.

Maadhimisho ya mwaka huu kitaifa yamefanyika Mkoani Simiyu na kaulimbiyu ikisema ‘’Badilika kuelekea jamii jumuishi na imara kwa wote’’.

SOURCE: ISSACK GERALD

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...