Thursday, 11 January 2018

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, ametangaza rasmi kuanza oparesheni ya kukamata watu wanaovaa nguo zisizo na heshima.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP Charles Mkumbo 

ARUSHA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo ametangaza rasmi kuanza oparesheni ya kukamata watu wanaovaa nguo zisizo na heshima kulingana na maadili ya Tanzania na kuwafikisha mahakamani.

Ameongeza kusema kuwa jamii imeathiriwa pakubwa na kuiga utamaduni wa magharibi ambao hata wao hufanya hivyo kutokana na hali ya hewa.

Katika siku za hivi karibuni suala hilo limezua mjadala mkubwa  miongoni wasanii wa muziki nchini  na jamii kuhusu Katazo la wanawake wanaojihusisha na sanaa kuvaa nusu utupu.

 Rais wa jamuhri ya Muungano wa Tanzania DK John Pombe Magufuli akiwa mjini Dodoma mwaka jana kuhudhuria mikutano ya CCM taifa alikemea vitendo hivyo na kuagiza vyombo husika vichukue hatua za haraka.


Chanzo:Tanzania Today

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...