Thursday, 11 January 2018

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA) imesema mikoa ya Lindi ,Mtwara na Morogoro kusini inatarajiwa kunyesha mvua kubwa inayozidi milimita 50 ndani ya saa 24 .

DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini(TMA) imesema mikoa ya Lindi ,Mtwara na Morogoro kusini inatarajiwa kunyesha mvua kubwa inayozidi milimita 50  ndani ya saa 24 .

Kwa mujibu wa TMA imesema mvua hizo zimeanza  usiku wa kuamkia leo na zinatarajiwa kumalizika  Januari 12 mwaka huu ambazo zitanyesha kwa kiwango cha juu cha asilimia 80

TMA imesema hali hiyo inatokana na kuimarika kwa ukanda wa mvua na mgandamizo mdogo wa hewa uliopo kwenye mkondo wa bahari wa Msumbiji.

Wakazi wa maeneo hayo wanashauriwa kuchukua tahadhari kutokana na mabadiliko hayo ya hali ya hewa.

Chanzo:Mwananchi 

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...