NSIMBO
Baadhi ya wakazi wa
Kata ya Katumba halmashauri ya Nsimbo wameitaka serikali kutoa tamko kuhusu
hatima ya nafasi ya Udiwani katika Kata hiyo kufuatia Diwani aliyekuwepo
kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela.
Wakizungumza na Mpanda
radio fm kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa nafasi ya Diwani kama msimamizi
mkuu wa shughuri za maendeleo haipaswi
kuwa wazi bila ufafanuzi wowote.
Mpanda radio fm
imemtafuta Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Raphael Karinga ili
atoleee ufafanuzi ikiwemo hatua walizo zichukua ambapo amedai kukabiliwa na
majukumu na kwamba atazungumza mara baada ya kuhitimisha majuku hayo.
Diwani wa kata hiyo
Seneta Baraka amefungwa tangu mwaka jana akidaiwa kupokea hongo kwa mfugaji
mmoja ili amuidhinishe kufanya shughuri za ufugaji katika eneo lililo zuiliwa
na Mahakama.
Chanzo: Alinanuswe Edward
No comments:
Post a Comment