Friday, 12 January 2018

Waziri wa mambo ya nje wa Guniea ya Ikweta Bw. Agapito Mba Mokuy amesema uasi uliozimwa mwishoni mwa mwaka jana ulipangwa nchini Ufaransa lakini serikali ya Ufaransa haihusiki.

Waziri wa mambo ya nje wa Guniea ya Ikweta Bw. Agapito Mba Mokuy


MALABO

Waziri wa mambo ya nje wa Guniea ya Ikweta Bw. Agapito Mba Mokuy amesema uasi uliozimwa mwishoni mwa mwaka jana ulipangwa nchini Ufaransa lakini serikali ya Ufaransa haihusiki.

Shirika la habari la Ufaransa lilimnukuu Bw. Mokuy akisema, nchi yake itashirikiana na Ufaransa kuanza uchunguzi baada ya kupata taarifa zaidi.

 Mpaka sasa wamluki 27 waliohusika na uasi huo wamekamatwa na wengine 150 wametoroka.

Bw. Mokuy amesema, kutokana na uasi huo, na pia haijakuwa tayari kikamilifu, Guniea Ikweta imesimamisha kwa muda kujiunga na makubaliano ya mawasiliano ya watu ndani ya eneo la katikati ya Afrika yaliyopitishwa na jumuiya ya uchumi na sarafu ya eneo hilo mwezi Oktoba mwaka 2017.


Chanzo: CRI

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...