Saturday, 6 January 2018

Mwandishi wa kitabu kijulikanacho Fire and Fury kinachoangazia mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump amesema alizungumza na Rais huyo wakati akikiandika kitabu hicho.


WASHINGTON DC

Mwandishi wa kitabu kijulikanacho Fire and Fury kinachoangazia mwaka wa kwanza wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump amesema alizungumza na Rais huyo wakati akikiandika kitabu hicho.

Kitabu hicho ambacho kimezua mihemko,kinakinzana na kauli ya Trump kuwa hajawahi kuzungumza na mwandishi huyo Michael Wolff na hakuwa ametoa idhini kwa mwandishi huyo kuingia Ikulu ya Rais ya White House.

Watu wengi wamekinunua kitabu hicho Fire and Fury kilichoanza kuuzwa jana,kikielezea maisha ya Trump na yanayojiri katika Ikulu ya Rais.

 Mawakili wa Trump wametishia kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mwandishi na mchapishaji wa kitabu hicho na wamejaribu kukizuia kuchapishwa na kutolewa.
Trump amekipuuzilia mbali kitabu hicho kinachomkashifu vibaya akisema kimejaa tu uongo mtupu.


Wolff amesema Trump hakuwa amejitayarisha kushinda uchaguzi wa Rais na kuwa kiongozi wa Marekani na kuwa wasaidizi wa Rais wanamuona kama mtoto na asiye na uwezo wa kuliongoza taifa.

No comments:

Featured post

MASIKINI WEEE!!!!! KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KATIKA KIWANJA CHA MPIRA AZIMIO

Na;Ezelina Yuda Mtoto mchanga mwenye jinsia ya Kike anayekadiriwa kuwa wa siku 1 ameokotwa akiwa hai kandokando ya uwanja wa azimio  ...