ADDIS ABABA
Serikali ya Ethiopia imewakamata watu 107 kwa
tuhuma za kuhusika na vurugu zilizotokea hivi karibuni katika eneo la mpaka wa
mikoa ya Somali na Oromia.
Kamishna wa tume ya polisi ya Ethiopia Abiyu
Assefa amesema watuhumiwa 98 kati ya hao waliokamatwa wanatokea mkoa wa Oromia
na wengine tisa kutoka mkoa wa Somali.
Mapigano makali katika eneo la mpaka wa mikoa
hiyo miwili yaliyotokea mwezi Septemba mwaka jana yalisababisha mapigano ya
kikabila yaliyosababisha vifo vya watu kadhaa.
Mbali na vifo hivyo vinavyotajwa kutokea
halikadhalika mamia ya watu walikimbia makazi yao wakihofia kuuwawa.
Chanzo:Radio China
No comments:
Post a Comment